Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa daraja la Tanzanite (Salander) jijini Dar es Salaam na kwamba ameridhishwa na kasi ya mradi huo.
Majaliwa amekagua ujenzi wa daraja hilo lenye urefu wa kilomita 1.03 na upana mita 20.5 linalogharimu Shilingi Bilioni 243.75 leo Desemba 22.
Daraja hilo linatarajiwa kukamilika Oktoba 14, 2021 “Nimekagua mradi na ujenzi wake unaendelea vizuri, sina mashaka na viwango na naamini utakamilika kwa wakati. Watanzania wanasubiri kwa hamu waanze kupita katika daraja hili,” Majaliwa.