Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema atapeleka Timu maalum ya uchunguzi Wilayani Kigoma ili ifanye uchunguzi wa fedha zinazopotea kinyemela kupitia mtandao wa Watumishi wasio Waaminifu.
“Hapa Manispaa mnapokea fedha, zinakaa kwenye akaunti kwa muda halafu zinapotea, hazijulikani zimefanya nini, nitaleta Timu, waje wafuatilie hapa Kigoma, waende hadi TAMISEMI ili tuone huo mnyororo unaenda wapi”
Ametoa kauli hiyo leo asubuhi Ijumaa, Septemba 22, 2023 wakati akiongea na Viongozi wa Dinj, Serikali, CCMna Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kwenye ukumbi wa NSSF, Kigoma mjini”