WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza taasisi za Serikali ambazo haziajaanza kutoa huduma kupitia vituo vya huduma pamoja vya Shirika la Posta Tanzania zijipange na zihakikishe zinaanza kutoa huduma katika vituo hivyo ndani ya mwaka huu wa fedha.
Amezitaja baadhi ya taasisi hizo kuwa ni Tume ya Ajira, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Maeneo Maalumu ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo wakati akizindia Vituo vya Huduma Pamoja vya Shirika la Posta Tanzania kwenye viwanja vya Posta Makao Makuu jijini Dar es Salaam. Huduma Pamoja ni vituo vitakavyotoa huduma zote za Serikali katika eneo moja kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma mbalimbali na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
BABA AKOPA MILIONI 10 RIBA YAPANDA ASHIDWA KULIPA WATOTO WALIA ”NYUMBA IMEUZWA TUMELALA NJE WIKI”