Top Stories

Waziri Mkuu atoa maelekezo kwa Wanafunzi waliorudi nchini kutokana na vita ya Ukraine (video+)

on

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Wanafunzi waliokuwa wanasoma katika Vyuo mbalimbali nje ya nchi ambao walirudishwa nchini kufuatia kuzuka kwa janga la UVIKO19 pamoja na kuibuka kwa vita kati ya Urusi na Ukraine wawasilishe taarifa zao Kamisheni ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).

Ametoa wito huo leo Alhamisi, Mei 12, 2022 wakati akijibu swali la Mbunge wa Hai, Saasisha Mafuwe katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Mbunge huyo alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia Wanafunzi hao kuendelea na masomo wakiwa hapa nchini.

Waziri Mkuu amesema ili kuhakikishia Wanafunzi hao wanasaidiwa kumaliza masomo yao wakiwa hapa nchini, Serikali inawataka wawasilishe taarifa zao TCU ambayo imeweka utaratibu unaoruhusu Wanafunzi hao kuhamisha viwango vya ufaulu wa masomo vitakavyowawezesha kuendelea na masomo yao nchini.

 

Tupia Comments