Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok amekamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa Wanajeshi nyumbani kwake baada ya Wanajeshi hao ambao hawajafahamika kuvamia makazi yake leo Jumatatu katika kile kinachotajwa kuwa ni jaribio la Mapinduzi ya Serikali.
Al Hadath TV inaripoti kwamba Kikundi hicho cha Wanajeshi kimemkamata Waziri Mkuu huyo na bado kinamshikilia kwenye makazi yake.
Wanajeshi hao wamewakamata pia Mawaziri wanne na Viongozi wengine wa ngazi za juu na sasa huduma za internet nchini Sudan hususani Katika Makao Makuu ya Nchi hiyo Khartoum zimekata.