Mix

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa azindua kiwanda cha Sika Tanzania

on

Leo Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amezindua rasmi Kiwanda kipya cha Sika Tanzania chenye mtambo wa kutengeneza mota na mtambo wa Admixture unaofanya kazi kikamilifu, Ghala na jengo la Utawala katika majengo yake Mbezi Salasala jijini Dar es Salaam.

Kampuni hiyo imedhamiria kuimarisha mnyororo wa usambazaji wa kemikali za ubora wa juu katika tasnia ya ujenzi.

Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na Waziri wa Biashara na Viwanda, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Mhe. Didier Chassot, na Meneja Mkuu wa Sika Tanzania, Dennis Ott.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alipongeza uwekezaji wa Sika katika Utafiti na Maendeleo, vitengo vya Uzalishaji, mauzo ya kiufundi na kazi za kiutawala, ambao unaonyesha mfano mzuri wa msingi bora wa ukuaji endelevu.

Kwa hiyo Sika haiwekezi tu katika ardhi, majengo, na mashine bali zaidi ya yote kwa Watanzania, akitaja Sika kama kipengele kidogo katika mageuzi ya jumla ya uchumi wa Tanzania kuelekea uchumi wa Viwanda.

Katika hafla ya uzinduzi huo Waziri wa Biashara na Viwanda aliahidi kuendelea kujenga sera zinazosaidia mazingira bora ya uwekezaji kutoka nje kukua na kuwanufaisha Watanzania wengi zaidi.

Katika uzinduzi huo, Meneja Mkuu wa Sika Tanzania, Dennis Ott alisisitiza kuwa Sika Tanzania itaendelea kupata imani kutoka kwa wadau wa sekta ya ujenzi wakiwa ni Taasisi za kiserikali, kampuni za ujenzi, washauri wa uhandisi, wasanifu majengo, wasambazaji na mafundi ujenzi.

Sika Tanzania inafuraha kuchangia katika ukamilishaji wa miradi ya kihistoria kama vile mradi wa Reli ya Standard Gauge, Uwanja wa Ndege wa JKN Terminal III, Mfugale Flyover, na Kituo cha Umeme wa Maji cha Julius Nyerere. “Bidhaa zetu zimetengenezwa nchini Tanzania kwa ubora wa Uswizi”.

Sika iwekeza kwenye mkakati wa ukuaji barani Afrika, ikiwa na operesheni katika nchi 18 na operesheni 10 za hivi karibuni zikiwa zimefunguliwa katika kipindi cha miaka 8 iliyopita, ikiwa na zaidi ya wafanyakazi 1200 wakizalisha bidhaa za ubora wa hali ya juu na kuwahudumia wateja kutoka katika viwanda 20 barani kote.

Sika Tanzania ilianza shughuli zake mwaka 2016 na kwa sasa inaajiri wafanyakazi 37. Inataraji kutokana na uzinduzi wa mtambo mpya na dhamira kubwa ya kupanua mtandao wa usambazaji wa bidhaa za Sika, fursa zaidi kwa Watanzania zitafunguka na Sika itaweza kuwahudumia wateja wetu wa Tanzania na nchi za jirani.

Sika AG, iliyoko Baar, Uswisi, ni kampuni inayofanya kazi kimataifa kutengeneza kemikali maalum zitumikazo kwenye tasnia mbalimbali. Sika inatengeneza na kusambaza bidhaa zitumikazo kwenye ujenzi wa majengo, miundombinu pamoja na kwenye viwanda vya utengenezaji (magari, mabasi, lori, reli, mitambo ya nishati ya jua na upepo, facade). Sika inaongoza katika utengenezaji wa nyenzo zinazotumiwa katika kuziba, kuunganisha, kufuta, kuimarisha, na kulinda miundo ya majengo na miundombinu kwenye ujenzi.

Miongoni mwa bidhaa za Sika kuna kemikali za kuchanganyia kwenye zege zenye viwango vya hali ya juu, chokaa au mota maalum, bidhaa za uzibaji, na gundi, mifumo ya uimarishaji wa miundo ya majengo/miundombinu, sakafu za viwandani pamoja na mifumo ya paa na ya kuzuia maji. Sika inajivunia kuwa na operesheni ndani ya nchi 100 ulimwenguni kote ikitimiza zaidi ya wafanyakazi 25,000 ambao wana hamasa ya kuunganisha wateja moja kwa moja na suluhisho za Sika na kuhakikisha mafanikio ya wadau wote. Sika ilizalisha mauzo ya takriban dola za Kimarekani bilioni 8.5 mnamo mwaka 2020.

Soma na hizi

Tupia Comments