Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mbunge waJimbo la Ruangwa ameishukuru kampuni ya Insignia Limited kupitia rangi zake za Coral Paints kwa kuidhamini timu ya Namungo FC iliyopo jimboni mwake kuelekea msimu mpyawa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
Akizungumza kwenye hafla ya kusaini makubaliano yaudhamini na uzinduzi wa jezi mpya kati ya kampuni yaInsignia Limited na uongozi wa timu ya Namungo katikauwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi siku yaJumanne usiku, Majaliwa amesema timu hiyo imejiandaavizuri ili kuleta ushindani msimu huu.
”Tumejiandaa vizuri na vijana ( wachezaji) sasa hivi wapokambini mkoani Arusha kwa ajlli ya kambi ya maandalizi, huku usajili ukifanyika kimya kimya,”
” Tunawashukuru sana Coral Paints kwa kutupa nguvu kubwaNamungo kuelekea msimu ujao ili tufanye vizuri katika ligina michuano ya kimataifa endapo tutamaliza msimu huukatika nafasi za juu kabisa,” amesema.
Katika msimu uliomalizika, Namungo ilimaliza katika nafasiya tano ikiwa na pointi 40 na kukosa tiketi ya kuiwakilishaTanzania katika michuano ya kimataifa ngazi ya klabu Afrika ambayo Tanzania itawakilishwa na Simba, Yanga katika Ligiya Mabingwa Afrika wakati Azam na Singida Fontain Gate zitacheza Kombe la Shirikisho.
Hata hivyo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema timuhiyo imeweka mipango madhubuti ikiwemo kuimarisha uhaiwa matawi ya wanachama na kutafuta vyanzo mbalimbali vyakujiingizia mapato ikiwemo kupitia mauzo ya jezi na sapotikubwa kutoka kwa wana Ruangwa wenyewe na wadauwengine mbalimbali wakiwemo Coral Paints ili wawezekufanya vizuri zaidi msimu huu.
Waziri Mkuu amesema licha ya nafasi mbili za juu kuwangumu kwa sababu mara nyingi zinashikiliwa na Simba naYanga, lakini amesema ana Imani Namungo, au ’ Wauaji waKusini’ kama inavyojulikana ipo siku iitatwaa ubingwa huo
”Zile nafasi mbili za juu zinaweza kuwa mgogoro kwetu, japokuwa tutapambana na ipo siku tutafanikiwa kutwaaubingwa na ndio malengo yetu,”
” Lakini nafasi hii ya tatu na nne huku hatuna wasiwasi nayo, hii tunaiweza na tutapambana kwelikweli ili tuchezemichuano ya kimataifa,” alisema Waziri Mkuu.
” Nguvu kubwa tunayoipata kutoka kwa wadhamini wetu namashabiki inazidi kutupa matumaini na ari ya kupambana,”.
”Tunawashukuru sana, mara ya kwanza mmetusaidiakukarabati uwanja na sasa mmekuja na udhamini ili kutupanguvu katika safari yetu ya mafanikio,”amesema Majaliwa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Insignia Isaac Kiwango ambaye hata hivyo hakuweka wazi thamani ya udhamini huo, alisema udhamini wa kampuni hiyo ni wa miaka mitatu na umejikita katika maeneombalimbali na utakuwa wenye maboresho.
Alisema kampuni yake imedhamini vifaa vya timu hiyoikiwemo jezi aina tano ambazo timu hiyo imezizindua ikiwani kwa ajili ya mechi za nyumbani, ugenini, kirafiki. kombe la Shirikisho na nyingine ya kuitangaza Namungo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Namungo, TwahaMpembenwe ambaye pia ni Mbunge wa Kibiti naye alisemawanataka kuona namungo inasonga mbele katika Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho na hata itakaposhiriki michuano yakimataifa.
Aliwataka mashabiki, wanachama na wapenzi wa Namungokuwa kitu kimoja na kwamba mshikamano wao ndiomafanikio ya timu hiyo.
Tayari Bodi ya Ligi imetangaza Agosti 15, kuwa ndio tareheya kuanza kwa Ligi Kuu msimu wa 2023/24 huku Yangaikitetea ubingwa wake iliyoutwaa kwa mara ya pili mfululizo.