Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda ametoa Rai kwa Watanzania kutobeza fursa za Uwekezaji zilizopo Nchini ikiwemo Uwekezaji katika Bandari, kwani Uwekezaji huo utachangia katika kuleta maendeleo kwa Taifa.
Pinda ametoa pongezi hizo alipotembelea banda la TPA katika Maonesho ya kitaifa ya Wakulima Nanenane 2023 yanayofanyika katika Viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya.
Aidha, Waziri Mkuu Mstaafu Pinda ameshauri elimu zaidi iendelee kutolewa kwa Wananchi kuhusu Uwekezaji huo.
Pinda pia ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa bandari Tanzania TPA, kwa Kushiriki Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima NaneNane 2023 na kutoa Elimu kwa Umma kuhusu huduma zinazotolewa na bandari.
Kwa upande wake Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania- TPA Nicodemus Mushi, amesema Mamlaka hiyo inaendelea na mipango ya kuboresha Bandari Nchini zikiwemo Bandari za Maziwa, kwa lengo la kuboresha huduma na kuongeza ufanisi zaidi katika Bandari hizo.