Top Stories

Waziri Mkuu Swedeni ajiuzulu ndani ya saa 12 tangu ateuliwe

on

Waziri Mkuu wa kwanza Mwanamke nchini Sweden Magdalena Andersson amejiuzulu nafasi hiyo ikiwa ndani ya saa 12 tu toka alipoteuliwa, imeelezwa kwamba kujiuzulu kwake kumetokana na Bajeti yake kushindwa kupitishwa na badala yake Wabunge wakaiunga kwa kuipigia kura bajeti iliyoandaliwa na upinzani.

Andersson amejijengea sifa ya kuwa mkweli na asiepindisha maneno wala misimamo yake ambapo hivi karibuni alipewa jina la Tingatinga “buldoza” na kituo cha TV cha Sweden kiitwacho SVT kutokana na misimamo yake na sifa zake. 

ULIPITWA? HII NI PIKIPIKI YA UMEME, UKICHAJI INAKUTOA DAR HADI BAGAMOYO, INAZIDI YA MAFUTA KWA FAIDA YA 40%+ 

Soma na hizi

Tupia Comments