Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema katika kipindi hiki dunia inapohangaika na magonjwa mbalimbali watanzania waendelee kuchukua tahadhari huku wakiondoa hofu kwani hii ni vita na serikali inaendelea kupambana.
Aidha, amewataka watanzania kuchukua tahadhari katika uvaaji wa barakoa kwa kujiridhisha na kufahamu barakoa unayovaa imetoka wapi ikiwezekana ni vyema kushona ya kwako.
“Mwanzoni tulisema tujiepushe kutumia barakoa za nje kwa sababu tulitaka wananchi wetu wawe salama zaidi, ila niwaombe Watanzania tuendelee kuvaa Barakoa zetu za asili zile za kushona kwa vitambaa. ukiwa kwenye Shughuli zako zinazojumuisha mikusanyiko vaa Barakoa yako ili kujikinga”Waziri Mkuu
“Tuna Magonjwa mengi, Malaria, UKIMWI, BP, Kisukari nk Wataalamu wetu walio kwenye hospitali, maabara wanaendelea na uchunguzi na kujikita katika kutoa huduma” Waziri Mkuu
“Nawashukuru Sana Viongozi wa Dini kwani wamesikiliza maombi Rais kuhakikisha tunafanya maombi kwa siku 3, tunafunga na kusali.” Waziri Mkuu Kassim Majaliwa