Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu siku ya Alhamisi alisema kuwa serikali yake haijajibu pendekezo la Marekani na Ufaransa la kusitisha mapigano kwa siku 21 na Hezbollah nchini Lebanon, na kuwaagiza wanajeshi kuendelea kupigana kwa “nguvu kamili.”
Pendekezo hilo, lenye lengo la kusitisha mzozo unaoongezeka katika mpaka wa Israel-Lebanon, bado halijashughulikiwa na Israel, kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Netanyahu.
“Ni pendekezo la Marekani na Ufaransa, ambalo waziri mkuu hata hajalijibu,” taarifa hiyo ilifafanua, na kuongeza kuwa Netanyahu ameamuru Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) “kuendeleza mapigano kwa nguvu zote.”
Netanyahu pia alisisitiza kwamba operesheni huko Gaza itaendelea hadi malengo ya vita ya Israeli yatimizwe kikamilifu.