Aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Kilosa, Morogoro Mustafa Mkulo ameshangazwa na baadhi ya watu kudai anataka kugombea ubunge katika jimbo la Kilosa huku akikanusha hana mpango wowote wa kugombea nafasi hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari mjini Morogoro katika salamu za mwaka mpya wa 2020 ikiwa ni sehemu ya kawaida yake kufanya hivyo kila mwisho wa mwaka, Mkulo amesema ajabadilisha maamuzi yake ya kutogombea nafasi ya ubunge na kushangwazwa na baadhi ya watu kudai anataka kuombea tena nafasi hiyo.
“Kuna watu wamekuwa wakidai nataka kugombea tena ubunge Kilosa hizi ni habari za uongo sina mpango wa kugombea ubunge sehemu yoyote ile hapa nchini “ amesema Mkulo.
Mkulo amesema bado anajivunia katika miaka 10 ya ubunge jimbo la Kilosa kwa kutekeleza ilani ya chama kwa kipindi hicho na Wana-Kilosa kuridhika na utendaji wake.
Aidha Waziri waziri huyo mtaafu wa Fedha amesema ataendelea kuwa mwanachama na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hata hivyo amefafanua kuwa pamoja sio mbunge na wala hafikirii kugombea nafasi hiyo lakini ataendelea kutoa mawazo yake kwa CCM na hata kusaidia wasiojiweza kwa niaba ya CCM ili chama kiweze kutekeleza mipango yake ya kimaendeleo.
Katika salamu zake za mwaka 2020 Mkulo amesema anafurahishwa na utendaji kazi mzuri wa Rais wa awamu ya tano Dkt John Pombe Magufuli na anaunga na wanaCCM wengi kutomuingilia katika katika uchaguzi wa kipindi cha pili ya miaka mitano ijayo 2020 hadi 2025 ili aweze kutekeleza kwa ufasaha mipango ya kimaendeleo alioicha katika awamu ya kwanza.
“Huu ni utaratibu wangu wa kila mwaka kutoa salaumu za mwaka mpya tangu nikiwa mbunge na sasa ni wakati wa kusema ukweli Rais Magufuri kwa miaka minne amefanya mengi mazuri anahitaji pongezi kutoka kwa Watanzania hasa katika kupandisha uchumi na kuboresha miundombinu ya nchi hii” amesema Mkulo.
Mustafa Mkulo ni Mbunge Mstaafu ambaye aliongoza kwa miaka 10 katika jimbo la Kilosa ambapo pia katika kipindi hicho alishika nafasi ya Waziri wa Fedha na kuacha kugombea mwenyewe kwa hiari yake katika uchaguzi 2015 na nafasi yake ikachukuliwa na Mbunge wa sasa Mbaraka Bawaziri ambapo amesema maamuzi yake ya kuacha kugombea ni kutoa nafasi wa wanaCCM wengine kuchangia mawazo yao katika kuliletea maendeleo Jimbo la Kilosa.
JAJI NSEKELA AZUNGUMZIA RAIS MAGUFULI KUWASILISHA TAMKO LA MALI NA MADENI