NI Waziri wa Fedha dkt. Mwigulu Nchemba ambae leo Agosti 20, 2021 amefafanua fedha zinazopatikana katika tozo na makato ya miamala ya simu jinsi zitakavyokwenda kutekeleza miradi mbalimbali.
Hapa nimekusogezea ufahamu alichokizungumza kuhusu kiasi cha fedha kilichokusanywa katika upande wa Mafuta.
“Kwa upande wa tozo ya mafuta kwa July, 2021 tumekusanya zaidi ya Tsh.Bilioni 28 ambazo ni mahususi kwa ajili ya Barabara ambazo hazipitiki na mwezi huu tutakusanya zaidi ya na Bil 20, kama ilivyo kwa tozo za miamala tuna uhakika na huku pia tutakuwa na zaidi ya Bil 48”-Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. Mwigulu Nchemba, Dar es Salaam
WAZIRI MWIGULU AFUNGUKA FEDHA ILIYOKUSANYWA KWENYE TOZO ZA WANANCHI “TUMEKUSANYA BILIONI 48”