Top Stories

Waziri Mwigulu asema “tutategemea kuwatoza kodi Google, Twitter, Facebook na nyinginezo”

on

NI Septemba 1 2021 ambapo Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu Nchemba alizungumza na Waandishi wa habari kuhusu viwango vya tozo kwenye miamala vilivyopunguzwa.

Aidha pia akagusia suala la Serikali kuanza kuwatoza kodi wamiliki wa mitandao ya kijamii ikiwemo Google, Facebook, Instagram, Twitter.

Akizungumza katika mkutano huo wa waandishi wa habari alisema…“Tunategemea (tunatafuta namna) kuwatoza kodi kama nchi zingine zinavyofanya kwa Wamiliki wa Google, Twitter, Facebook, Instagram, apple na Makampuni mengine kwasababu haya ni Makampuni ya Kimataifa na yanapata fedha kwa Watu wetu na hayalipi kodi, kodi za mitandao hazihusishi Watumiaji (wananchi wanaotumia mitandao hiyo) hivyo Watu wasipotoshe” ——— Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango.

BREAKING: TOZO ZASHUSHWA, AGIZO LA RAIS SAMIA LATEKELEZWA,MWIGULU ATIA SAINI MAREKEBISHO YA KANUNI

Soma na hizi

Tupia Comments