Waziri wa Elimu, Sayansi na Technolojia, Profesa Joyce Ndalichako pamoja na balozi wa China hapa nchini,Wang Ke leo wameshiriki uwekaji wa jiwe la msingi la sekondari ya mfano ya masomo ya Sayansi mkoani Arusha iliyopewa jina la mkuu wa mkoa huo Mrisho Gambo.
Shule hiyo ya kisasa ambayo kwa mkoa wa Arusha ya kwanza itakayokuwa ikiendeshwa kwa mfumo wa kisayansi (STEM)yaani SAYANSI,TEKNOLOGIA,UHANDISI,NA HISABATI, Ipo katika kata ya Olasity jijini ambayo hadi sasa tayari madarasa manane ya kisasa yamekamilika na tayari wanafunzi wamenza kuyatumia.
Shule hiyo pia ina Maabara nne za kisasa, chumba cha Kompyuta, nyumba za walimu na madawati ambapo madarasa mengine na jengo la utawala bado vikiendelea kujengwa.
Akizungumza baada ya kutembelea na kukagua shule hiyo waziri Ndalichako amepongeza jitihada za uongozi wa mkoa wa Arusha kwa mikakati yake ya kuboresha elimu mkoani humo na nchi nzima ambapo amesema kama serikali wanataka shule hiyo kuwa ya mfano hapa nchini kwa kuwa itakuwa na uwezo wa kuchukuwa wanafunzi wa Sayansi kwa kiasi kikubwa hivyo kusaidia kupata wataalam wakutosha katika Sayansi na technolojia.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ametumia fursa hiyo kuwashulkuru wadau wote walioshiriki kufanikisha ujenzi wa shule hiyo kwa nanma moja ama nyingine na kusema kuwa kama mkoa wameamua kuwekeza katika elimu kutokana na kutambua umuhimu wa elimu huku akiwatoa hofu wale wote wanaodhani amekuwa akifanya maendeleo hayo kwa nia ya kutaka ubunge wa jiji la Arusha.
Ilikufanikisha ujenzi wa shule hiyo wadau mbalimbali wamechangia katika nyanja mbalimbali ambapo Benk ya I & M imechangia madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni kumi.
Akizungumza katika hafla hiyo Afisa mtendaji Mkuu wa Benki ya I&M Baseer Mohammed amesema Benk hiyo imekuwa ikitoa sehemu ya faida yake kusaidia jamii.
“Mhe waziri I & M bank leo imetoa madawati haya 100 kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli za kutoa elimu bure ili watoto wengi waweze kunufaika na elimu bure” >>> Baseer
Mbali na wadau hao ikiwemo ubalozi wa China pia Benk ya CRDB imejenga darasa moja katika shule hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 20.
Meneja wa benki ya CRDB Kanda ya kaskazini Chiku Issa amesema benki hiyo imekuwa na desturi ya kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu,Afya,na nyinginezo.
Leo Benk ya CRDB imekabidhi darasa lenye thamani ya shilingi milioni ishirini na ikiwa ni kuunga mkono jitihada za mhe Rais za kutoa elimu bure alisema Chiku.