Waziri wa Habari, Mawasiliano na teknolojia ya Habari Mhe. Jerry Silaa amemtaka mtendaji mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kuhakikisha anasimamia ujenzi wa mnara yote 758 nchini Ili wananchi waweze kupata Huduma ya mawasiliano.
Mhe. Silaa ameyasema hayo akiwa katika ziara ya siku moja Kijiji cha Msolokelo kata ya Pemba Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ambapo Kijiji hicho ni moja ya eneo lenye changamoto ya mawasiliano.
Mhe Silaa anasema lengo la Serikali kuhakikisha wananchi wanaindokana na adha ya kupata changamoto ya mawasiliano hivyo lazima minara yote ambayo tayari fedha zimetengwa tangu mwaka 2023 na kutakiwa kukamilika mei mwaka 2025 inakamilika Kwa wakati
Kwa Upande wake Mtendaji mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Mhandisi Peter Mwasalyanda amesema Kwa mkoa Morogoro una minara 69 ambao baadhi imekamilika,na mingine ipo Kwenye hatua mbalimbali za kukamilika .
Amesema changamoto ya kukosa mawasiliano Kwa Kijiji hicho ni kutokana na jiongrafia kwani tayari mradi wa ujenzi wa mnara umekamilika ambao umejengwa Kijiji vha Pemba hivyo watalazimika kuweka minara miwili ndani ya kata moja ili huduma hiyo iweze kuwafikia wananchi.
Naye Mbunge wa Jimbo la Mvomero Jonas Vanzeland amemshukuru Rais Samia Kwa kumpatia minara 15 katika Jimbo hilo.
Mhe. Zealand amemuomba Dokta Samia kuendelea kuleta fedha za miradi ya maendeleo Katika Jimbo hilo ikiwemo sekta afya,elimu barabara na umeme ambao tayari umeshafika
Awali baadhi wakazi wa Kijiji hicho akiwemo Ally Jumanne amesema kwa Sasa wanalazimika kupanda juu ya miti au milima Ili waweze kufanya mawasiliano.
Anasema hali hiyo imekuwa kikwazo hasa katika masuala ya biashara na Maendeleo kwa ujumla kwani wanalazimika kusafiri umbali mrefu Ili kupata huduma hiyo.
Amesema hata baadhi ya watumishi wa Serikali wameshindwa kukaa katika eneo hilo kutokana na Kukosa mawasiliano na kuomba uhamisho mara tu wanaporipoti katika vituo vya kazi ikiwemo, watendaji,walimu na Madaktari.