Waziri wa mawasiliano na Teknolojia ya Habari ameongoza kikao kazi cha pili serikalini na wadau wa sekta ya mawasiliano na teknolojia ya habari kuhusu utekelezaji wa mkakati wa taifa wa uchumi wa kidigitali 2024/2034 kilicho fanyika hii leo jijini Arusha.
Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Silaa ameeleza Mafanikio ambayo kama wizara wamefikia ikiwemo ufikishwaji wa mkongo wa mawasiliano ya taifa, kukua kwa huduma za simu kiganjani , kupungua kwa garama za kupiga simu na kuwezesha huduma za kidigitali kuwafikia wafanyabiashara wengi.
Aidha katika kikao hicho Waziri Silaa akafanya uzinduzi wa kampeni ya kupambana na kuzuia utapeli kwenye mtandao kampeni ijulikanayo kama SITAPELIKI. yenye lengo la kutoa elimu kwa jamiii hususani katika kushuhulikia maswala ya utapeli na ulaghai mtandaoni. huku akihimiza wananchi kuwa na amani katika kututumia mtandao
Pia amewahimiza wananchi juu ya utaratibu wa kuwasilisha malalamiko yao kwa watoa huduma kuwa ni kupitia namba 100 pekee kwa mitandao yote au kwa malalamiko mengine wafike ofisi za TCRA.na Baada ya uzinduzi akatoa rai kwa Kila mdau kutekeleza kwa wakati mpango huo mahususi kwa kuelimisha jamiii jinsi ya kujikinga na udanganyifu wa mitandaoni
Kwa upande wake Miraji Mtaturwa mwakilishi wa mwenyekiti wa kamati bunge miundominu na mawasiliano na teknolojia akashauri Kuimarisha uwezo wa data, Malipo ya kidigitali, pamoja na Garama za bando ili kutoa urahisi wa huduma na kuweza kuwafikia wananchi wote hadi wa hali za chini.
Aidha ameongeza kuwa kupitia kikao hicho wanatarajia kulenga upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kuchochea uchumi wa kidigitali kwa kuwezesha miundombinu ya kidital, Utawala na mazingira wezeshi, Uelewa wa kidigital na ujuzi,Utamaduni wa maendeleo ya teknolojia pamoja na kukuza ushirikishwaji wa huduma za kidigitali
NaeKatibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Mohammed Khamis Abdulla Akaeleza kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau wameweza kufanya utekelezaji wa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano ambapo hadi sasa umefikia asilimia 50 huku minara 304 imeongezwa nguvu kutoka 2G kwanda 3G, 4G na 5G ambapo utekelezwaji huo umefanikiwa kufanyika kwa asilimia 100.
Aidha akieleza mafanikio mengine wameweza kupeleka WIFI katika maeneo ya umma na mashuleni nchini, na kukamilisha majadiliano kati ya serikali na watoa huduma za mawasiliano ambapo inatarajiwa umoja wa watoa huduma wa mawasiliano kukabidhi miundombunu ya mkongo wa mawasiliano wa serikali pamoja na kusaini mkataba na serikali.
Baaada ya kikao kazi hicho kutaandaliwa maazimio ya utekelezaji wa pamoja kati ya sekta ya umma na sekta binafsi, na mpango wa kufanya utafiti ufuatiliaji pamoja natathimini.