Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Lusubilo Mwakabibi (pichani) baada ya kupokea malalamiko na tuhuma za mwenendo usiofaa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Tamisemi, Waziri Ummy ametoa agizo hilo leo Aprili 25, 2021 huku akitaja sababu nyingine ya kusimamishwa kwa Mkurugenzi huyo kuwa ni matumizi mabaya ya madaraka.
“Waziri Ummy amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Lusubilo Joel Mwakabibi baada ya kupokea malalamiko na tuhuma za mwenendo usiofaa, matumizi mabaya ya madaraka, ubadhirifu na usimamizi usiorihisha wa miradi ya maendeleo katika halmashauri ya Manispaa ya Temeke kutoka kwa wananchi, viongozi na vyanzo vingine.
“Kufuatia tuhuma hizo, waziri Ummy amemuagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais –TAMISEMI kupeleka timu za uchunguzi mara moja,” imeeleza taarifa hiyo.