Top Stories

Waziri Ummy apokea msaada wa vifaa toka China “tunapima wenye dalili” (+video)

on

Ubalozi wa China nchini Tanzania umeipatia Serikali msaada wa vifaa kinga kwa ajili ya kuendelea kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19 (Corona), na kuahidi kuendelea kushirikian na Serikali ya Tanzania kukabiliana na ugonjwa huo, hadi hapo utakapomalizika.

Akipokea vifaa hivyo Waziri Ummy Mwalimu amesema msaada huo utaenda kwa watumishi wa afya kote nchini kwani serikali imetoa kipaumbele cha kwanza kwao ili kuweza kuwakinga na maambukizi ya Covid-19.

“Kwa niaba ya serikali tunaishukuru sana Serikali ya China kwa mchango huu, na niendelee kuwathibitishia wale wote mnaoisaidia Serikali ya Tanzania, msaada huu tutaupeleka kwa watumishi wa afya, kipaumbele ni kuwakinga watumishi wa afya wasipate maambukizi” Ummy

Ummy Mwalimu amesema msaada huo uliotolewa na ubalozi wa China nchini Tanzania ni pamoja na mavazi (PPE) 1,000 ya kujikinga wakati wa kuhudumia watu waliothibitika kuwa na ugonjwa wa corona, Barakoa (Mask) 100,000 pamoja na Vipima joto vya mkono(thermal scanner) 150.

“WALIOPO LOCKDOWN WANAJUTA” WAZIRI AKIKAGUA KIWANDA CHA MASK

Soma na hizi

Tupia Comments