Top Stories

Waziri Ummy awataka Ma-RC, DC kufanya kazi wasisubiri PDF ya uteuzi

on

Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu amewataka Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuendelea kuchapa kazi kama awali na sio kukaa kusubiria uteuzi.

Waziri Ummy ameyasema hayo katika ziara yake Wilayani Chemba Mkoani Dodoma kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na Kamati ya Fedha pamoja na Menejimenti ya Halmashauri hiyo.

“Hali inayoendelea kwa Viongozi hawa haileti Afya, wengine hawafanyi kazi eti wanasubiria mkeka, hamuoni kuwa mnaonea wananchi kupata haki yao ya msingi ya kuhudumiwa?” Waziri Ummy

“Kipindi hiki mnatakiwa kuendelea kuchapa kazi kama kawaida Wananchi wanahitaji kuendelea kuhudumiwa, suala la mkeka unakuja lini hilo ni kuliachia Mamlaka, ninyi chapeni kazi na mumtangulize Mungu Mbele” Ummy

RAIS SAMIA AFUTA KAZI MABOSS WATATU, AVUNJA BODI

Soma na hizi

Tupia Comments