Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu amesema yapo malalamiko kuwa baadhi ya Walimu wanaojitolea wanawasilisha barua feki zinazosema wanafanya hivyo wakati hawajitolei.
Ametoa kauli hiyo leo Mei 25, 2021 Bungeni Dodoma wakati akimjibu Mbunge wa Longido aliyehoji ni kwanini Seikali isiajiri Walimu ambao wanajitolea.
Amesema hata Wanaojitolea watafanyiwa uchambuzi ili kuona kama ni kweli wanafanya hivyo akiongeza, kigezo kikubwa kitakachotumika katika utoaji wa Ajira ni hicho.
Ameeleza, suala hilo ni tete ambapo nafasi ni 6,949 ilihali mpaka Mei 23, 2021 walioomba ni 89,958. Ameomba Serikali iaminiwe akisisitiza Haki itatendeka.
“Nimpongeze mheshimiwa Kiruswa kwa swali lake la nyongeza kuwa kwa nini tusiajiri walimu wanaojitolea lakini nataka kukiri yapo malalamiko hata hao wanaojitolewa kuna wengine wameleta barua feki za kusema kwamba wanajitolea wakati hawajitolei”Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu
“Jana mheshimiwa Spika tumepokea pia maelekezo yako, suala hili ni tete nafasi ni 6949 mpaka juzi walioomba wameshafika 89,958 kwa hiyo suala hili Serikali tutatenda haki hata hao wanaojitolea tutawachambua kama ni kweli wanajitolea”-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu
UKWELI WA TUKIO LA MWANAFUNZI KUSHAMBULIWA KWA VIBOKO SHULENI