Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ametii agizo la Rais Samia na kufika eneo la kwamsisi wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Ambapo baada ya kuona video iliyochapishwa na mwandishi wa habari Mbarouk Khan ikionesha wananchi wakiteseka kwa kukosa maji Rais Samia alitoa maagizo kwa Waziri kushughulikia changamoto hiyo haraka sana
Baada ya kufika Waziri aweso Amemtaka mkandarasi anayehusika kuomba radhi kwa wananchi pia amewataka wakandarasi wote nchini kuacha kuzoea matatizo ya wananchi