Waziri wa mambo ya nje wa Israel anaripoti baadhi ya maendeleo kuelekea kusitisha mapigano, licha ya Hezbollah kusema haijui lolote kuhusu hilo.
Waziri mpya wa mambo ya nje wa Israel alisema Jumatatu kwamba kumekuwa na “maendeleo fulani” katika juhudi za kumaliza mapigano na Hezbollah ya Lebanon.
Lakini msemaji wa kundi hilo la wapiganaji amesema kuwa halijapokea pendekezo lolote rasmi na liko tayari kuanzisha vita vya muda mrefu iwapo itahitajika.
Utawala wa Biden umetumia miezi kadhaa kujaribu kupanga makubaliano ya kusitisha mapigano, na kulikuwa na ripoti kwamba mjumbe wa Merika Amos Hochstein anaweza kurejea katika eneo hilo katika siku zijazo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Gideon Saar alisema makubaliano yoyote yatalazimika kujumuisha mifumo ya utekelezaji ili kuzuia Hezbollah kuunda upya miundombinu yake ya kijeshi karibu na mpaka.