Ziara hii inakuja baada mwenzake wa Ukraine, Dmytro Kuleba kufanya ziara barani Afrika.
Inatarajiwa kuwa huenda kiongozi huyo akakutana na rais wa Kenya William Ruto amabye hajaungana na viongozi wengine wa Afrika katika hafla ya kuapishwa kwa rais mteule wa Nigeria Bola Tinubu hii leo Jumatatu.
Sergey Lavrov amefanya mkutano na uongozi wa Bunge la Kenya mjini Nairobi.
Ukurasa wa Twitter wa Ubalozi wa Urusi nchini Kenya, umeandika kuwa itakuwa ni wiki ya mafanikio kati ya Kenya na Urusi.
Awali kiongozi huyo alikutana na spika wa bunge la kitaifa nchini Kenya Moses Wetangula afisini mwake.
Lavrov amekuwa akifanya ziara katika mataifa ya Afrika katika siku za hivi punde, matukio ambayo wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa huenda ni njia moja ya Urusi kutafuta mbinu za kupata ushawishi barani Afrika.