Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro amejiuzulu nafasi yake ya Uenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya Leseni za Vilabu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Katika barua aliyomuandikia Rais wa TFF Wallace Karia, Waziri Ndumbaro amefikia maamuzi hayo ili kupata nafasi ya kutekeleza majukumu yake mapya ya Uwaziri wa Michezo.
Itakumbukwa August 30, 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan alimteua Dkt. Damas Ndumbaro kuwa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo.