Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega leo amewasilisha Bungeni Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2023/ 2024 ambapo amesema uzalishaji wa nyama umeongezeka kwa 4.3% kutoka tani 769,966.7 mwaka 2021/2022 hadi tani 803,264.3 mwaka 2022/2023 huku uzalishaji wa maziwa ukiongezeka pia kutoka lita bilioni 3.4 mwaka 2021/2022 hadi kufikia lita bilioni 3.6 mwaka 2022/2023 sawa na ongezeko la 5%.
Ulega amesema “Vipande vya ngozi milioni 14.1 vimezalishwa mwaka 2022/2023 ikilinganishwa na vipande milioni 13.6 vilivyozalishwa mwaka 2021/2022, uzalishaji wa mayai umeongezeka kutoka mayai bilioni 4.9 mwaka 2021/2022 hadi bilioni 5.5 mwaka 2022/2023 sawa na ongezeko la 12.2%”
“35% ya kaya zilizopo nchini zinajishughulisha na ufugaji, kati ya hizo 39.3% wanafuga ng’ombe, 36.2 % wanafuga mbuzi, 13.5% wanafuga kondoo na 10.9% wanafuga nguruwe, aidha 55.4% ya kaya hizo pia hujishughulisha na ufugaji wa kuku”
View this post on Instagram