Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: Agizo la Waziri Mkuu kuhusu posho zinazotolewa na wakurugenzi wa halmashauri
Share
Notification Show More
Latest News
Tazama Shaka alivyokula kiapo cha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa “Sitotoa siri”
January 27, 2023
Mapya ndoa ya Dr Mwaka haijavunjwa, tamko kali latolewa na baraza la Ulamaa
January 27, 2023
Mkali Brand TZ kutokea Bongo Flevani kaachia hii EP yake mpya, isikilize hapa
January 27, 2023
Mkali Lord Eyez ametuletea hii collabo yake akiwa na Adiana Ross
January 27, 2023
Picha: Mwili wa Mtanzania aliefia kwenye vitani urusi, waagwa kwa picha nyumbani kwao
January 27, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Mix > Agizo la Waziri Mkuu kuhusu posho zinazotolewa na wakurugenzi wa halmashauri
Mix

Agizo la Waziri Mkuu kuhusu posho zinazotolewa na wakurugenzi wa halmashauri

January 3, 2017
Share
2 Min Read
SHARE

Leo January 03 2017 Waziri mkuu Kassim Majaliwa amefanya ziara yake ya kikazi katika wilaya ya Kigamboni ambapo amezungumza na watumishi wa manispaa ya Kigamboni na kuagiza wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuhakikisha fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya posho mbalimbali zisizokuwa za kisheria zinaelekezwa katika miradi ya maendeleo.

‘Kuanzia sasa marufuku Wakurugenzi kutoa posho zisizotambulika kisheria zikiwemo za mazingira magumu, kujenga uwezo na vitafunwa katika halmashauri zenu na badala yake fedha hizo zitumike kwenye miradi ya maendeleo’;-Waziri Majaliwa

‘Katika halmashauri zetu kila mtumishi anashiriki katika ukusanyaji wa mapato hadi walinzi, lakini mwisho wa siku vitafunwa huliwa na wachache wanaojiita wakubwa huku wengine wakisikilizia kwa nje, jambo hili haliwezekani’-Waziri Majaliwa

Waziri Mkuu amesisitiza kwamba Mkurugenzi yeyote atakayebainika kulipa posho hizo baada ya siku ya leo  atakuwa amejifukuzisha kazi.

Imeelezwa kwamba agizo hilo litawezesha Jiji la Dar es Salaam kuokoa sh bilioni 130 zilizokuwa zitumike na Halmashauri na Manispaa za jiji hilo, ambazo kwa sasa zitaingizwa kwenye miradi na shughuli za maendeleo.

Aidha, ameagiza fedha zilizokuwa zikitolewa kwa madiwani kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo zisitolewe moja kwa moja kwa madiwani na badala yake  zipelekwe kwenye kata husika na zifuatiliwe matumizi yake.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amezionya halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa kila fedha inayopelekwa kwenye halmashauri hizo inatumika kama ilivyokusudiwa na atakayebainika kutumia kinyume hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Wakati huo huo waziri Mkuu ametoa siku tatu kwa watumishi 10 wa halmashauri ya Kigamboni ambao wamehamishiwa kutoka wilaya ya Temeke wawe wameripoti katika Manispaa hiyo, vinginevyo watakuwa wamejifukuzisha kazi.

VIDEO: ‘Hakuna mchango mwingine utakaoletwa ofisi ya waziri mkuu unaohusu Kagera’;-JPM, Bonyeza play hapa chini

You Might Also Like

Fredy Lowassa akabidhi vifaa vya shule kwa waliofauli 2023

Gynah ni mwimbaji wa kimataifa kenye usiku wa Kahawa

PICHA: Jerry Muro akabidhi madarasa 29 kwa RC Singida

Samsung wafungua duka lao ndani ya Palm village Mikocheni

Hatimaye Miss Tanzania 2020 akabidhiwa zawadi yake

TAGGED: Waziri mkuu Majaliwa
Edwin Kamugisha TZA January 3, 2017
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article VIDEO: Alichozungumza kocha Mayanja kabla ya Simba kucheza dhidi ya KVZ
Next Article Nigeria yaanza kutekeleza mpango wa kuwapa fedha kila mwezi raia wake
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Tazama Shaka alivyokula kiapo cha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa “Sitotoa siri”
Top Stories January 27, 2023
Mapya ndoa ya Dr Mwaka haijavunjwa, tamko kali latolewa na baraza la Ulamaa
Top Stories January 27, 2023
Mkali Brand TZ kutokea Bongo Flevani kaachia hii EP yake mpya, isikilize hapa
Entertainment January 27, 2023
Mkali Lord Eyez ametuletea hii collabo yake akiwa na Adiana Ross
Entertainment January 27, 2023

You Might also Like

Entertainment

Mkali Brand TZ kutokea Bongo Flevani kaachia hii EP yake mpya, isikilize hapa

January 27, 2023
Entertainment

Warembo wanaounda kundi la Tango Supreme kutumbuiza Dar, 27th Jan Elements Masaki

January 27, 2023
Entertainment

Mabibi na Mabwana Nuh Mziwanda ametuletea hii single mpya ‘Nikizipata’

January 26, 2023
Entertainment

PROFILE: Mfahamu Vido Vidox, ripota wa Ayo TV kwa stori za mastaa!!

January 26, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?