Zaidi ya Wahariri 130 kutoka vyombo mbalimbali vya Habari nchini wanatarajia kukutana Mkoani Morogoro katika Mkutano wa kujadili masuala mbalimbali ya kitaaluma.
Akizingumza na wanahabari mjini Morogoro Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri TEF Neville Meena amesema kuwa katika Mkutano huo mada takriba Sita zitawasilishwa.
Meena amesema kuwa miongoni mwa mada zitakazo wasilishwa katika Mkutano huo ni pamoja na maadili katika vyumba vya Habari na upunguaji wa wanawake katika sekta ya Habari.
Anasema kwa hivi sasa Waandishi wanawake wengi wamekuwa wakirudi nyuma katika masuala ya Habari hivyo katika mkutano huo itawasilishwa mada ya wanawake.
Mkutano huo unatarajiwa kuanza Machi 29 mwaka Huu Hadi Machi 31 mwaka Huu mjini Morogoro.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mkutano huo anatarajiwa kuwa waziri wa Habari Nape Nauye huku mgeni maalum akiwa ni waziri wa katiba na sheria dokta Damasi Ndumbaro.