Moja ya stori ambayo inakamata headline ni oparesheni inayoendelea kufanywa na TRA kugakua vituo vya mafuta na kuvichukulia hatua ambavyo havitoi risiti za elektroniki zilizofungwa moja kwa moja kwenye pampu za mafuta maarufu kama ‘EFPP’.
Hadi sasa TRA imevifunga vituo vingi vya mafuta Mwanza kutokana na kutofuata sheria na taratibu zilizoamriwa ambapo Ayo TV na millardayo.com zinaye Katibu Mahusiano na Mawasiliano wa Chama cha Wauza Mafuta Rejareja TAPSOA Kanda ya Ziwa Ahmed Misanga.
>>>”Toka jana vituo vingi vya mafuta vimefungwa sana na TRA kutokana na kutokutumia mashine ya EFPP. Mashine ya EFPP ni mashine ambayo inatoa risiti automatic kutoka kwenye pampu ya maputa unapouza. Wauzaji wengi wa mafuta wamekuwa wakitumia mashine za EFD.” – Ahmed Misanga.
Mtanzania aliyewahi kuweka rehani gari lake kumsadia kijana ada ya Shule!!!