Top Stories

INAFURAHISHA: Kilichowatokea mapacha wa kike wanaofanana Marekani

on

Katika hali ya kushangaza mapacha wawili wa kufanana wa kike Rachael McGeoch and Beccy Pistone wenye miaka 34 wamejifungua siku moja na katika hospitali moja Marekani huku wakieleza kuwa ukaribu wao tangu wakiwa watoto ulifanya wataniane mara kadhaa kuwa inawezekana wakaja kuzaa siku moja.

Mapacha hao ambao pia wapenzi wao wanaitwa Willium wamejikuta wanajifungua katika vyumba vya hospitali vinavyofuatana kwa kupishana tu masaa machache baada ya mmoja wao kuwa amefikisha muda wa kujifungua siku chache zilizopita lakini ikashindikana kujifungua hadi alipokuja pacha wake kumwona ndipo wote wawili walipo shikwa na uchungu na kujifungua.

“Baada ya jitihada za madaktari kujaribu kunichoma sindano ya uchungu ili nijifungue kwa siku mbili na kushindikana, tulijua tunahitaji kuwa pamoja na baada tu ya pacha wangu kuja Boston kuniona niliweza kupelekwa chumba cha kujifungulia na kujifungua.” – Rachael McGeoch

Image result for Rachael McGeoch and Beccy Pistone with their fiances

Ulipitwa na hii?Diamond kamtibua tena Zari?? hii comment imeibua mapya

Hii je?Ni kweli Diamond anatoka kimapenzi na mshindi wa BBA?

Soma na hizi

Tupia Comments