Michuano ya Club Bingwa Afrika hatua ya pili imeendelea leo kwa michezo kadhaa kuchezwa, Mabingwa wa Ligi Kuu soka Tanzania bara Dar es Salaam Young Africans walikuwa Lusaka Zambia katika uwanja wa Taifa wa Mashujaa kuwania nafasi ya kuingia hatua ya makundi kwa kucheza dhidi ya Zanaco.
Yanga ambao mchezo wa kwanza ulichezwa Dar es Salaam na kulazimishwa sare ya 1-1, waliingia Zambia wakiwa na lengo moja la kuhakikisha wanasonga mbele hatua inayofuata kwa kupata ushindi katika mchezo huo au sare ya kuanzia 2-2 na kuendelea.
Sare tasa ya 0-0 inaiondoa Yanga katika michuano ya Club Bingwa Afrika dhidi ya Zanaco kwa kujikuta game ikimalizika kwa sare tasa, hivyo Yanga sasa anaangukia katika michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kutolewa kwa kuruhusu kufungwa goli nyumbani katika mchezo wa kwanza uliyomalizika kwa sare ya 1-1.
PICHA KWA HISANI YA @shaffihdauda
ALL GOALS: Simba vs Yanga February 25 2017, Full Time 2-1