Habari za Mastaa

Waliodaiwa kunyanyaswa kingono na R.Kelly wajitokeza kumtetea (+Video)

on

Inaelezwa kuwa kupitia mahojiano ya kituo cha TV cha CBS “This Morning” kimefanya mahojiano na wasichana wawili ambao wanatajwa kuwa waliwahi kuwa mapenzini na mwimbaji R. Kelly na kusema kuwa chochote kinachozungumzwa juu ya mwimbaji huyo ni uongo.

Kupitia mahojiano hayo msichana mmoja aliyefahamika kwa jina la Azriel Clary alisema kuwa baba yake mzazi alimtaka adanganye kuhusu umri wake pamoja na kutengeneza kanda za ngono pamoja na R.Kelly ambapo baadae wangezitumia kwa kulipiza kisasi.

Wasichana hao walisisitiza na kusema kuwa wazazi wao waliwataka wafanye hivyo ili baadae watumie picha pamoja na videos hizo kama ushahidi endapo R.Kelly angegoma kutoa kiasi cha pesa walichokitaka huku lengo lao kubwa ilikua kukusanya pesa kutoka kwa R. Kelly .

“Kwa mara ya kwanza nilipokutana na R. Kelly alijua nina miaka 18 lakini nilipokuwa na miaka 17 wazazi wangu walitaka nipige picha na R.Kelly na kuchukua video za ngono na vitu kama hivyo na walisema wakitaka kumtishia watatumia picha pamoja na videos kama ushahidi”

MAJONZI: MWILI WA EPHRAIM KIBONDE UMEAGWA MWANZA NA KUSAFIRISHWA

Soma na hizi

Tupia Comments