Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Real Madrid imemtangaza mbadala wa Zidane

on

Ni siku 12 zimepita toka aliyekuwa kocha mkuu wa club ya Real Madrid ya Hispania Zinedine Zidane atangaze kujiuzulu nafasi hiyo, leo uongozi wa club ya Real Madrid wametangaza mbadala wa Zidane.

Club ya Real Madrid leo imemtangaza rasmi Julen Loptegui kuwa ndio kocha wao mkuu baada ya Zidane kuondoka, Julen Loptegui atajiunga na Real Madrid baada ya kumalizika kwa majukumu yake ya kuiongoza timu ya taifa ya Hispania katika fainali za Kombe la dunia 2018 nchini Urusi.

Zidane

Julen Loptegui anarudi Real Madrid kwa mara ya kwanza baada ya miaka 9, mwaka 2008-2009 alikuwa kocha wa timu ya Real Madrid BJulen Loptegui hata hivyo amewahi kuzifundisha timu mbalimbali kama Rayo Vallecano na FC Porto.

FULL VIDEO: Zilivyotolewa tuzo za MO Simba Awards 2018

Soma na hizi

Tupia Comments