Mix

‘Marufuku kupita kwenye barabara za Mwendokasi’- Mambosasa

on

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limetoa onyo kwa madereva wa Serikali na madereva wa magari ya watu binafsi kuacha mara moja kupita kwenye barabara ambazo ni maalum kwa magari ya mwendokasi na kusisitiza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na oparesheni ya kukamata vyombo vyote vya moto vinavyopita kwenye barabara hizo na dereva yeyote atakayekamatwa atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kamanda Mambosasa amesema kuanzia September 19, 2019 wameendesha oparesheni maalum ya kukamata magari yanayopita kwenye barabara za mwendokasi ambapo katika oparesheni hiyo jumla ya magari 50 yamekamatwa, magari 19 ni mali ya Serikali na magari 31 ni ya watu binafsi.

ULIMISS HII YA RAIS MAGUFULI KUTANGAZA UTEUZI UZITO ITAZAME HII VIDEO HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments