May 24 couple ya mastaa Kim Kardashian na Kanye West walitimiza mwaka mmoja wa ndoa yao tangu walipofunga mwaka jana Italy.
Wawili hao walitumia nafasi hiyo kuweka kwenye mitandao picha mbalimbali za harusi yao ambazo hazikuwahi kuonekana.
Mbali ya picha hiyo Kanye West leo aliamua kuweka ujumbe mzuri kwenye ukurasa wake wa Twitter ambao ulikua maalum kwa ajili ya mkewe pamoja na mwanae, North West.
Ujumbe ulisomeka hivi..; >>> “Kim, I’m so happy to be married to the girl of my dreams… I love you and Nori so much!!! I would find you in any lifetime“>>> @
Kim aliiona post hiyo, nae akajibu; >>> “Awwww baby I love you so much!!!!!! I would find you too! Anywhere!!!!“>>>@
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.