Michezo

Labda Samuel Eto’o atakwenda Arsenal ?!!

on

Screen Shot 2014-05-31 at 2.07.12 AMIkiwa wiki hii ndio inaishia, kwenye kumbukumbu ya stori nilizokutana nazo na nikashawishika kuzisoma ni pamoja na hii ya Samuel Eto’o ambae mkataba wake na Chelsea umemalizika na sasa ni mchezaji huru.

Gazeti la Miror ni miongoni mwa vyombo vya habari vilivyoandika kwamba staa huyu ameonyesha nia ya kuichezea Arsenal kuanzia msimu ujao akiwa na nia ya kutaka kumthibitishia Jose Mourinho kwamba bado yuko ngangari.

Pamoja na kwamba hawa wanasema mwakilishi wa Eto’o ndio kathibitisha kwamba mchezaji huyo kasema yuko tayari kwenda kwa Wenger, bado sijaamini asilimia 100 mpaka nimsikie au kumuona yeye mwenyewe akiongea….  acha tusubirie.

Ila unavyoona anaweza kuongeza kitu kweli akijiunga na Arsenal mtu wangu?

Tupia Comments