Michezo

UCL: Welbeck ang’ara, haya ndio matokeo ya Arsenal vs Galatasary

on

article-2776817-21DBC84D00000578-233_964x386Mshambuliaji mpya wa Arsenal aliyetokea kwenye klabu ya Manchester United, Danny Welbeck jana usiku aliandika  historia mpya katika michuano ya ligi ya mabingwa wa ulaya.

Akiitumikia klabu yake ya Arsenal kwa mara ya pili kwenye michuano hiyo, Welbeck aliungana na washambuliaji Mike Newell, Andy Cole (mara mbili), Alan Shearer, Owen (mara mbili) and Rooney – kuwa wachezaji pekee raia wa Uingereza ambao wamewahi kufunga hat trick katika michuano ya ulaya.

Welbeck alianza kufunga magoli mawili katika kipindi cha kwanza kabla ya Alexis Sanchez kuongeza la 3 na kuiwezesha Arsenal kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa magoli 3-0.

Kipindi cha pili Welbeck alifunga goli la 4 – na kutimiza magoli matatu kwenye mechi, ikiwa hat trick yake ya kwanza katika maisha yake ya soka la ushindani. Burak aliifungia Galatasary goli la kufutia machozi kwa mkwaju wa penati.

Mpaka mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho Arsenal walikuwa wameshinda 4-1.

Tupia Comments