Ikiwa leo ni siku ya kusherehekea miaka miwili ya kuzaliwa kwa Lola, Mtoto wa Whozu aliyezaa na Tunda, imefanyika sherehe fupi ambayo Wema Sepetu ameandaa kwa ajili ya Mtoto huyo ambaye kwa sasa anaishi na Wema na Whozu.
Wema na Whozu wamefunguka kwa pamoja kuhusu malezi ya Mtoto huyo ambapo Wema amesema anampenda sana Lola na haoni kama kuna shida kwa Mama yake Tunda na ndio maana ameweza kuishi nae na hata kumpost.
Kwa upande wa Whozu amesema anafurahi kumuona Wema akiishi vizuri na Mtoto huyo.