Habari za Mastaa

“Msituwekee picha zenu zenye mistari ya ujauzito” – Wema Sepetu

By

on

Ni kawaida kwa baadhi ya wanawake hasa mastaa kupiga picha wakati wa ujauzito kwa ajili ya kumbukumbu zao na wakati mwingine kutokana na mapenzi waliyonayo kupiga picha ambapo mastaa mbalimbali wa kike duniani wamekuwa wakifanya hivyo.

Jambo hilo pia tumekuwa tukilishuhudia hata hapa Tanzania na baadhi ya mastaa pia wameshawahii kupiga picha za namna hiyo na wakati mwingine kuziweka kwenye mitandao ya kijamii jambo ambalo baadhi ya watu linawakera.

Wema Sepetu ni mmoja wa watu ambao wameonesha kukerwa na kitendo hicho akisema ni ukiukwajii wa maadili ya kiafrika na watanzania kwa ujumla na kuutumia ukurasa wake wa Instagram  kumpongeza muigizaji wa Bongomovie Esha Buheti baada ya kupiga picha akiwa mjamzito ndani ya mavazi ya kumsitiri.

Wema ameongeza kwa kusema kuwa ameshakubaliana na hali yake ya kutoweza kupata mtoto lakini hiyo haimzuii kusema yanayomkera kuhusiana na mambo ya uzazi.

Yaani ni Hivi, Hakunaga Jipya Now Mwaweza nitukana nikashtuka… Maana mi mwenyewe nishajikubali hali yangu… Labda niulize tu, Niko peke yangu nilokosa mtoto au ambaye sijazaa…??? HAPANA…!! Soooooooo Back to The Main Point, Nilichosema na nitakachoendelea Kusema, MUACHE KUTUWEKEA MIPICHA YA MITUMBO YENU YENYE MSTARI WA UJAUZITO… Yaani inshort, Muache kupiga picha za UTUPU kwenye Maternity Shoot zenu…. @esha.s.buheti Nakupenda mama…. You are the Definition of Womanhood & Motherhood… Na unajua Utamaduni wetu nini unataka…. Haya Wazungu endeleeni na Uzungu wenu…. Tukaneni na hapa pia…. Eti u thought I would keep quite jus cause mmeniita Jina nilolizoea… So nisi speak my Heart… Y’all are Very Funny….!!!! ??? Allah akutangulie kipenzi changu…. Baby Shower Loading…. @esha.s.buheti @esha.s.buheti @esha.s.buheti @esha.s.buheti @esha.s.buheti ….

A post shared by Wema Sepetu (@wemasepetu) on

Video: Gabo na Wema Sepetu wametuletea filamu mpya inaitwa KISOGO>>>

Soma na hizi

Tupia Comments