Michezo

Wenger amkataa Robin van Persie

on

Kocha wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger amefichua siri kuwa Robin Van Persie ambaye aliondoka Arsenal 2012 na kujiunga na Man United, alimpigia simu 2015 na kuomba arudi Arsenal lakini Wenger alimkatalia.

“(Van Persie) alinipigia simu 2015 kwa sababu alitaka kurudi (Arsenal) lakini ilikuwa haiwezekani, alikuwa anaelekea kumaliza soka lake na sisi (Arsenal) tulikuwa tumewekeza kwa wachezaji wachanga”>>> Wenger VIA Mirror

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Robin van Persie alijiunga na Arsenal 2004 akitokea Feyenoord ya kwao Uholanzi na kudumu na Arsenal kwa miaka nane (2012) kisha kujiunga na Man United, uhamisho ambao uliwakwaza sana mashabiki wa Arsenal.

Soma na hizi

Tupia Comments