Michezo

Ni kweli Arsene Wenger ana kinyongo na Liverpool? kauli yake ipo hapa

on

Kocha wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger ambaye mwaka 2013 alikuwa na dhamira ya dhati ya kuwania saini ya mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Liverpool Luis Suarez kwa dau la poundi milioni 40, alikuwa yupo tayari kulipa ili Liverpool imuuzie nyota huyo.

arsene-wenger_2390067b-620x388-23

Mwaka unaofuatia Liverpool walimuuza Suarez katika klabu ya FC Barcelona ya Hispania, August 24 Arsene Wenger amenukuliwa na vyombo vya habari kuwa hawasikitikii Liverpool kumkosa Raheem Sterling kwani hata yeye bado ina muumiza kutouziwa Suarez.

Arsene-Wenger

“Liverpool wapo katika nafasi ambayo wanaweza kufanya maamuzi yao wenyewe, walikataa kutuuzia Suarez hivyo siwezi kujisikia huzuni sana kwa ajili yao, binafsi kiwango cha Sterling tutakiona kwa muda mrefu sifikirii kama Sterling alifanya drama zozote hicho ndicho kilichotokea katika dirisha la usajili”>>>Sterling

Ikumbukwe kuwa vilabu vingi vya Ulaya hususani vinavyoshiriki Ligi moja huwa havipendi kuuziana wachezaji kwani wanaamini hawawezi kukupa silaha halafu uje huwafunge wenyewe. Hata suala la Peter Cech kujiunga na Arsenal Jose Mourinho alikuwa hajarizia na angependa kuona Peter Cech anacheza nje ya Uingereza.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments