Michezo

Siku moja kabla ya mchezo dhidi ya Olympiakos, Arsene Wenger kawaambia hili wachezaji wake..

on

Kocha wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger ambaye anaingia uwanjani na timu yake ya Arsenal akiwa katika mchezo wa pili wa Kundi F, katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya klabu ya Olympiakos katika Uwanja Emirates ambao ndio uwanja wa nyumbani wa klabu ya Arsenal.

2CDB76CF00000578-3251995-image-a-23_1443440440486

Arsene Wenger ambaye anaingiza kikosi chake uwanjani kikiwa na kumbukumbu sio nzuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza ugenini kwa goli 2-1 dhidi ya Dinamo Zagreb. Hivyo kocha Arsenal amewaambia wachezaji wake ni lazima kushinda mechi yake ya pili dhidi ya Olympiakos ili kujiwekaka katika nafasi nzuri.

2CDB570500000578-0-image-a-6_1443439723062

Wenger amezungumza na kikosi chake wanatakiwa kufanya jitihada ili kushinda mechi yake ya Jumanne ya September 29, taarifa hizo zinakuja ikiwa sambamba na kurejea kwa kiungo wake Francis Coquelin ambaye alikuwa majeruhi ila ameanza mazoezi September 28. Huenda kocha huyo anapatwa na wasiwasi kama akipoteza mechi yake dhidi ya Olympiakos inaweza ondoa hali ya kujiamini katika mechi yake ijayo dhidi ya FC Bayern Munich.

2CDB641000000578-0-image-a-17_1443439767597

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE

Tupia Comments