Michezo

Arsene Wenger anafikiria kuhusu kustaafu? Huwa inamjia akilini, alafu…

on

arsene_wenger_arsenal-374136

Kocha wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger amedumu na klabu ya Arsenal kwa zaidi ya miaka 15 toka alipojiunga nayo 1996, Wenger anakuwa kocha wa pili katika historia ya Ligi Kuu Uingereza kudumu na timu kwa muda mrefu baada ya kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson ambaye amestaafu mwaka 2013.

Arsene_Wenger_and_Sir_Alex_Ferguson_PicGetty_188214616

Wenger kushoto akiwa na Ferguson

Kufuatia kustaafu kwa Sir Alex Ferguson mwaka 2013 kumekuwa na maswali mengi kuhusiana na Wenger lini atastaafu, wengi wanaamini Wenger alikuwa na uwezo wa kuifundisha Arsenal kutokana na rekodi alioweka ndani ya miaka tisa ya mwanzo klabuni hapo, Wenger alishinda mataji 7 lakini miaka kumi baadae Wenger ameishia kutwaa mataji mawili pekee rekodi inayotia mashaka kuhusu uwezo wake kwa sasa.

ArseneWenger_3032530 (1)

Wengi walitazamia kuwa kuna uwezekekano wa Wenger kustaafu kwa miaka ya hivi karibuni lakini alichojibu kuhusu suala la yeye kustaafu bado linawaacha watu njia panda ya lini atastaafu.

“Kustaafu? ndio wakati mwingine huwa inanijia akilini lakini sio zaidi ya sekunde 5 kwa sababu huwa nahofia…Nataka nifanye vizuri na klabu ili siku nitakapoondoka niiache klabu katika nafasi nzuri ili iweze kuendelea poa”>>>Wenger

LONDON, ENGLAND - OCTOBER 26:  Arsene Wenger, manager of Arsenal looks on during the Barclays Premier League match between Crystal Palace and Arsenal at Selhurst Park on October 26, 2013 in London, England.  (Photo by Shaun Botterill/Getty Images)

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments