Wakati zikiwa zimebaki siku chache kabla ya timu yake kusafiri kwenda Allianz Arena kucheza mchezo wa pili wa hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa wa ulaya dhidi ya Bayern Munich, kocha Arsene Wenger ameisifu klabu ya Real Madrid na kusema ndio timu anayoipa nafasi ya kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa wa ulaya na anaamini wapinzani wake Bayern sio hatari kama walivyokuwa msimu uliopita.
Arsenal walifungwa na Bayern 2-0 mwezi uliopita katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora katika dimba lao la Emirates.
Pamoja kuwa moja ya timu inayotisha zaidi barani ulaya lakini Wenger ana maoni tofauti dhidi ya kikosi cha Pep Guardiola: “Msimu uliopita, Ribery na Robben walikuwa wakicheza pamoja na walikuwa kwenye kiwango kizuri sana, hivyo Bayern walikuwa hatari sana kwenye kushambulia,
“Mwaka huu wanatisha sana katika kumiliki mpira, lakini nadhani hawana hatari sana katika kufunga – Nadhani tuliona hilo katika mchezo dhidi ya Arsenal. Pamoja na kucheza wachezaji 10 hawakuweza kutufunga mabao mengi.”
Real walifunga Schalke 6-1 wiki iliyopita, wapo kwenye kilele cha La Liga na wapo katika fainali ya Copa del Rey.
Na Wenger anasema kikosi hicho cha Carlo Ancelotti ndio kina nafasi ya kubeba ubingwa wa Champions League.
Mfaransa: “Real Madrid wapo kwenye kiwango kizuri sana. Kwangu mimi hii ndio timu iliyokamilika zaidi katika kila idara. .”