Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kutakua na ongezeko la joto kali katika baadhi ya maeneo ya Tanzania kufuatia kuwepo kwa hali ya unyevunyevu angani na jua kuwa la utosi.
TMA imeyataja maeneo yatakayoathirika zaidi kuwa ni Ukanda wa Pwani DSM, Tanga, Unguja na Pemba yanayotarajiwa kuwa na kiwango cha juu cha joto cha nyuzijoto 32 hadi 34.
Mkurugenzi Mkuu TMA, Dkt. Agnes Kijazi amesema vipindi vya joto kali vinatarajiwa kuendelea kuongezeka mwezi February 2020 wakati jua litakapokuwa la utosi.
TAZAMA BASHE AKIMUOMBEA MZUNGU ALIYEPIGWA BEI NA TANESCO “WANATAKA MILIONI 90”