West Ham United imekuwa eneo la karibu zaidi kwa winga wa Brazil Anthony, huku nia rasmi ya timu hiyo ya Uingereza kupata huduma ya mchezaji huyo ikithibitishwa Januari hii.
Ripoti zinaonyesha kuwa Manchester United iko tayari kumtoa Anthony kwa mkopo mwezi huu baada ya kipindi kigumu kwake Old Trafford, ambacho kinafungua milango kwa vilabu vingi vinavyovutiwa, haswa Real Betis na Marseille.
Ingawa vilabu vingine vinashindana kumjumuisha ila kwa sasa West Ham wanaonekana kuongoza mbio hizo, hata hivyo, timu hiyo inakabiliwa na changamoto ya jinsi ya kumuunganisha Anthony na Mohamed Quddus katika nafasi moja, jambo ambalo linazua maswali kuhusu muundo wa timu iwapo dili hilo litakamilika.
Anthony, ambaye alijiunga na Manchester United akitokea klabu ya Ajax ya Uholanzi kwa dau kubwa, hakufanikiwa kutoa kiwango alichotarajia kwenye Ligi Kuu ya England, na kutokana na kushuka kwa kiwango chake ilionekana wazi kuwa mchezaji huyo alihitaji mazingira mapya kujenga upya maisha yake ya soka.