Michezo

West Ham wapo kwenye mazungumzo na mashabiki wao

on

Club ya West Ham United ya England ipo kwenye mazungumzo na mashabiki wake kuona namna ya kutengeneza atmosphere uwanjani wakati wa mechi zao za kumalizia msimu 2019/20 zitachezwa bila mashabiki.

West Ham wanataka mashabiki wao wawe wanaonekana na kushangilia mechi uwanjani kupitia Live Video Chat (Zoom Software) ambayo itaongeza hamasa za kelele za mashabiki uwanjani lakinj wakitokea nyumbani.

Vilabu mbalimbali duniani vinatarajia kutafuta njia ya kuongeza mvuto katika Ligi zao za soka wakati huu zikichezwa bila mashabiki wakimalizia msimu wa 2019/20 sababu ya Corona, baadhi ya mpango ni kucheza sauti za mashabiki zilizorekodiwa katika mechi zilizopita ili kuendelea kuleta hamasa.

Soma na hizi

Tupia Comments