Michezo

West Ham yamfungia shabiki sababu ya MO Salah

on

Club ya West Ham United ya England leo imetangaza kumfungia kwa miaka mitatu kuingia uwanjani shabiki wake Bradley Thumwood kwa kosa la kumbagua Mohamed Salah wa Liverpool katika mchezo dhidi yao February 2019.

Shabiki huyo alinaswa na Camera akitamka maneno ya kumbagua na kumdhihaki MO Salah kwa kutumia dini yake kwa kumwambia”Salah you f****** Muslim”

Katika mchezo wa soka ubaguzi wa namna yoyote ile rangi, dini havikubaloki, Bradley amekiri kutenda kosa hilo na kujutia kitendo hicho ambacho kimekuwa kikipingwa ndani ya soka na nje ya soka.

Soma na hizi

Tupia Comments