Habari za Mastaa

Hali si shwari ndoa ya Kanye West na Kim Kadarshian…

on

kanye-west-kim-kardashian-vogue-2

Ndoa ya mastar wawili kwenye anga la Holywood nchini Marekani Kanye West na Kim Kadarshian imeripotiwa kuwa hatarini kutokana na hali ya Kanye kutotimiza majukumu ya ndoa.

Watu wa karibu na familia ya wawili hao wamesema Kim Kadarshian siku za hivi karibuni amekuwa hana raha kutokana na Yeezy kupoteza hamu ya kuwa naye karibu kutokana na kuwa ‘busy’ na kazi zake za kimuziki na masuala mengine.

Kim Kadarshian amemtaka mumewe kuhudhuria darasa maalum la ushauri nasaha kwa wanandoa ili kuokoa ndano ya changa.

Kim Kadarshian, Kanye West na mtoto wao, North.

Mitandao ya habari za udaku ikiwemo TMZ na The National Enquirer imeandika kuwa Kim Kadarshian amemtaka mume wake kuhudhuria darasa maalum la ushauri nasaha kwa wanandoa ili kuweza kurudisha uhusiano wao katika mstari kabla hali haijawa mbaya zaidi na kusababisha kuvunjika kwa ndoa yao.

Tupia Comments