Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) amewataka watanzania kutotumia lugha za matusi kukosoa jitihada mbalimbali zinazofanywa na Rais wa Serikali ya Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Waziri Nape ameyasema hayo Julai 18 Mkoani Dar es Salaam alipokuwa akizungumza Katika Kongamano la Majadiliano ya Ripoti ya Tume ya Haki Jinai lililohudhuriwa na Wataalamu, Viongozi Wastaafu, Watumishi wa Serikali na Wanafunzi.